Wednesday, 25 February 2015

UBAKAJI NI UNYAMA USIO KIFANI



UBAKAJI NI UNYAMA USIO KIFANI

Ni jambo la kusikitisha kugundua kwamba utekelezaji wa unyama huu bado umekita mizizi katika karne ya ishirini na moja, ambapo watu wameelimika kupitia mfumo mpya wa teknolojia ya kisasa almaarufu ‘digital’.

Kufuatia kifo cha msichana moja aliyebakwa na kuuawa katika chuo kikuu cha Moi, hofu na taharuki zimezuka chuoni humo. Miongoni mwa waliohadhirika zaidi kutokana na kisa hicho ni wanafunzi wa kike ambao wanahofia usalama wao. Hii imewafanya kutotoka nje usiku hivyo basi kuchangia kuzoroteka kwa masomo yao  kwani hawaendi maktaba masaa ya usiku kwa kuhofia maisha yao. Wafanyi biashara nao wameadhirika hadi wanalazimika kufunga biashara zao mapema kutokana na ukosefu wa usalama katika maeneo ya kituo cha magari kijulikanacho kama “stage” na cheboywo.

Juhudi za serikali na jamii kwa ujumla kukabiliana na jinamizi hili la ubakaji zimeambulia patupu. Habari zinazo chipuka kwenye vyombo vya habari  ni zile za ubakaji na mauaji. Kusema kweli, watu wamekosa nidhamu na intidhamu hadi wakabakiwa na unyama wa kupindukia. Heshima na taadhima kwa binadamu wenzao zimeadimika kama maziwa ya kuku. Hadi lini tutaacha kusikia habari za baba kumdhulumu bintiye kingono?Ni lini wasichana wa umri mdogo wataacha kunajisiwa na watu wazima? Ni nani kawakamua utu uzima?

Ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha kuona baadhi ya  wale uwapendao wakipitia dhuluma za ubakaji. Wasichana wa chini ya umri wa miaka kumi na sita hubakwa mara kwa mara na kulazimishwa kubaki kimya kwa tishio la kifo lakini wanawake wa umri wa miaka kumi na nane  na kuendelea wanaelewa haki zao, hivyo basi kuuawa baada ya kunajisiwa haswaa wanapowatambua wavamizi hao.Kinachoshangaza ni kwamba wanaume hao wanapokamatwa na kufikishwa kortini, hudai kwamba wanawake hawa huwa hawavalii  mavazi ya heshima. Jambo dhahiri ni kuwa hawawezi kupata utamu wowote kutoka kwa mwanamke huyo kushinda utamu wa wake wao au wapenzio.

Wanawake wanashauriwa wawe waangalifu maanake mambo kangaja huenda yakaja na unayedhani mwendani wako anaweza kugeuka na kuwa adui wako. Usalama utaanza miongoni mwetu, iwapo tutashirikiana kwa pamoja kuangamiza uhalifu.

3 comments:

  1. Why do bad things happen to bad people? why do bad thing happen? this Question have bagged my mind since i so them happen to a friend of mind.

    ReplyDelete
  2. It is said "usalama unaanza n Wewe mwenyewe" choose your friends wisely. It's sad to here that bad things happen to good people so so sad.

    ReplyDelete
  3. lets stay safe. security begins with me.

    ReplyDelete