UBAKAJI NI UNYAMA USIO KIFANI
Ni jambo la kusikitisha kugundua kwamba utekelezaji wa
unyama huu bado umekita mizizi katika karne ya ishirini na moja, ambapo watu
wameelimika kupitia mfumo mpya wa teknolojia ya kisasa almaarufu ‘digital’.
Kufuatia kifo cha msichana moja aliyebakwa na kuuawa katika
chuo kikuu cha Moi, hofu na taharuki zimezuka chuoni humo. Miongoni mwa
waliohadhirika zaidi kutokana na kisa hicho ni wanafunzi wa kike ambao
wanahofia usalama wao. Hii imewafanya kutotoka nje usiku hivyo basi kuchangia
kuzoroteka kwa masomo yao kwani hawaendi
maktaba masaa ya usiku kwa kuhofia maisha yao. Wafanyi biashara nao wameadhirika
hadi wanalazimika kufunga biashara zao mapema kutokana na ukosefu wa usalama
katika maeneo ya kituo cha magari kijulikanacho kama “stage” na cheboywo.
Juhudi za serikali na jamii kwa ujumla kukabiliana na
jinamizi hili la ubakaji zimeambulia patupu. Habari zinazo chipuka kwenye
vyombo vya habari ni zile za ubakaji na
mauaji. Kusema kweli, watu wamekosa nidhamu na intidhamu hadi wakabakiwa na
unyama wa kupindukia. Heshima na taadhima kwa binadamu wenzao zimeadimika kama
maziwa ya kuku. Hadi lini tutaacha kusikia habari za baba kumdhulumu bintiye
kingono?Ni lini wasichana wa umri mdogo wataacha kunajisiwa na watu wazima? Ni
nani kawakamua utu uzima?
Ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha kuona baadhi ya wale uwapendao wakipitia dhuluma za ubakaji.
Wasichana wa chini ya umri wa miaka kumi na sita hubakwa mara kwa mara na
kulazimishwa kubaki kimya kwa tishio la kifo lakini wanawake wa umri wa miaka
kumi na nane na kuendelea wanaelewa haki
zao, hivyo basi kuuawa baada ya kunajisiwa haswaa wanapowatambua wavamizi
hao.Kinachoshangaza ni kwamba wanaume hao wanapokamatwa na kufikishwa kortini,
hudai kwamba wanawake hawa huwa hawavalii
mavazi ya heshima. Jambo dhahiri ni kuwa hawawezi kupata utamu wowote
kutoka kwa mwanamke huyo kushinda utamu wa wake wao au wapenzio.
Wanawake wanashauriwa wawe waangalifu maanake mambo kangaja
huenda yakaja na unayedhani mwendani wako anaweza kugeuka na kuwa adui wako.
Usalama utaanza miongoni mwetu, iwapo tutashirikiana kwa pamoja kuangamiza
uhalifu.
Why do bad things happen to bad people? why do bad thing happen? this Question have bagged my mind since i so them happen to a friend of mind.
ReplyDeleteIt is said "usalama unaanza n Wewe mwenyewe" choose your friends wisely. It's sad to here that bad things happen to good people so so sad.
ReplyDeletelets stay safe. security begins with me.
ReplyDelete